Mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ametangaza rasmi nia ya kuwania urais wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi mbele ya umati wa watu waliofurika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha na kutaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kupambana na umaskini,kulinda rasilimali za nchi na kuwaunganisha watanzania .
Mh.Lowassa ambaye aliingia.uwanjani akisindikizwa na msafara wa pikipiki na magari pia amesema akipewa fursa atahakikisha anadumisha muungano.
Amesema ataweka misingi imara ya kuharakisha maendeleo mazuri kwa wananchi na kuwawezesha vijana kuondoa tabaka la walionacho nawasionacho.
Awali viongozi wa dini na siasa akiwemo kingunge Ngombale Mmwiru wameseama Lowassa ana sifa za kiongozi anayefaa kuliongoza taifa kwa sasa.
Sherehe hizo zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka kona mblimbli nchini burudani kubwa ilikuwa ni Helkopta ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Bw. Joseph Msukuma.