Jumanne, 31 Machi 2015

Hispania Katika Mtihani Wa Machungu Ya 2014

Waliokua mabingwa wa dunia mwaka 2010, timu ya taifa ya Hispania hii leo watapambana na mahasimu wao wakubwa kwa sasa timu ya taifa ya Uholanzi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Mchezo huo utakua unakumbusha hisia za maumivu kwa mashabiki wa Hispania ambao bado wanaungulia kipondo cha mabao matano kwa moja walichokipokea wakati wa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi Guus Hiddink, amesema hauchukulii mchezo huo kama sehemu ya uhasama zaidi ya kuamini ni mpambano wa kuwapima wachezaji wake ambao wana mlima mrefu wa kupanda kuelekea nchini Ufaransa zitakapochezwa fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2016.
Amesema anatambua ulimwengu wa mashabiki wa soka unasubiri na kuona nani atakua mbabe dhidi ya mwenzake na wengine wanaamini huenda ikawa sehemu ya kulipiza kisasi, lakini kwake hajali suala hilo hata kama itatokea kikosi chake kinaanguka kwa kufungwa na Hispania.
Kwa upande wa  kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi Vicente del Bosque González, hakutofautiamna sana na mpinznai wake kwa kusisitiza jambo la kutofikiria matokeo ya mabao matano kwa moja aliyokutana nayo wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Del Bosque amesema soka ni mchezo wa makosa anakubali wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, alifanya makosa na akakubali kipigo hicho kitakatifu, lakini amewataka mashabiki wa soka duniani kote kusahau yaliyopita na kuutazama mchezo wa hii leo kama mchezo wa kawaida.
Katika mchezo huo Uholanzi inatarajia kuwakosa wachezaji wake muhimu Arjen Robben pamoja na Robin van Persie ambao wanaendelea kuuguza majeraha.
Hispania wataingia uwanjani hii leo wakiwa na kumbu kumbu ya ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata dhidi ya Ukraine wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, ili hali Uholanzi watakuwa na kisulisuli cha matokeo ya bao moja kwa moja dhidi ya Uturuki.
Uhasama baina ya mataifa hayo uliibuka mara baada ya matokeo ya mchezo wa fainali katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 iliyofanyika nchini Afrika kusini ambapo Hispania walitwaa ubingwa baada ya kuwabwaga Uholanzi kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri.