Jumapili, 5 Julai 2015

KAJUNA CUP LEO NDIO LEO FAINALI ZIKIPIGWA KATIKA VIWANJA VIWILI TOFAUTI

Leo ni fainali ya kajuna cup katika viwanja vya shule ya msingi mbata kati ya timu ya kijiji cha ghana Ghana fc wakichuana vikali na timu ya mbeya veterani.kumbuka timu zote hizi mbili ni timu bora kabisa mpaka kufikia leo fainali ,ghana fc wanajivunia fainali kalribu zote wameshiriki kwa hiyo wao kwa mchezo wa leo wanatambua wanachokihitaji ni kukabidhiwa kombe na fedha taslimu,kwa upande wa timu ya Mbeya veterani wao wanasema kazi yao ni moja tu kupata ushindi dakika tisini wamesema watatumia uzee wao kuweza kuwapa mashabiki burudani safi kabisa kwani hata wapinzani wao wanajua .