Kocha msaidizi wa mbeya city Mohamed kijuso na Msemaji wa Klabu ya Mbeya city Dismas ten wameanza kupata wakati mgumu kutoka kwa Mashabiki wa timu yao.Kijuso anatuhumiwa kuwa anabagua wachezaji wa Mbeya na kuwapa nafasi wachezaji wa Dar.Msemaji wa Timu Dismas mashabiki wanamlalamikia kuwa anashindwa kutumia nafasi yake ya kuweka Propoganda za kimichezo kama Wasemaji wengine wa Vilabu wanavyokuwa wanazipromoti timu zao.hayo yamefanyika baada ya mchezo kumalizika kati ya Mbeya City na Wenda Fc ambapo City waliibuka na ushindi dhidi ya Wenda Fc.