Jumapili, 3 Mei 2015
JKT RUVU , NDANDA FC NA PRISONS WASHINDA
Timu ya JKT Ruvu imeondoka kwenye mstari wa kushuka daraja baada ya jana kuibuka na ushindi wa goli 1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya Mgambo Shooting.
Katika mchezo huo JKT Ruvu walipata goli lao pekee katika dakika ya 11 kupitia kwa Ally Bilali na goli hilo kudumu kwa dakika zote 90 za mchezo.
Kama ilivyo ada kwa michezo inayo chezwa katika uwanja wa Mkwakwani kutawaliwa kwa mipira mirefu, hali hiyo iliendelea kujitokeza huku eneo la kuchezea likiwanyima uhuru wachezaji wa timu zote mbili.
JKT Ruvu jana walionekana kuwa hatari zaidi wakifika langoni mwa wapinzani kuliko Mgambo shooting, huku ubovu wa uwanja ukipilekea kukosekana magoli ya kutosha .
Katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Nangwanda sijaona umeshuhudia Ndanda FC wakiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Kagera sugar na kuifanya Ndanda FC kupata matumaini ya kubakia katika ligi kuu ya vodacom.
Katika uwanja wa Sokoini jijini Mbeya, mchezo uliowakutanisha wana Mbeya, Mbeya city na Tanzania Prisons umemalizika kwa Tanzania Prisons kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lilofungwa katika dakika za mwisho za mchezo.