Licha ya kucheza kwenye jua kali kufuatia uwepo wa mchezo wa Bonanza maalumu la mahakama kwenye uwanja wa Karume, kikosi cha Mbeya City Fc Imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji JKT Ruvu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
City iliunza mchezo huo kwa kasi ikijenga mashambulizi kutoka eneo la katikati ya uwanja lililokuwa likiongozwa na Kenny Ally pamoja na Rafael Daud, waliokuwa wakiunganisha vyema Haruna Moshi na Ditram Nchimbi kwenye safu ya ushmbuliaji, ilifanikiwa kuandikisha bao la kwanza kupitia Hassan Mwasapili ayeuunganisha mpira uliokuwa umepigwa na Ramadhan Chombo Redondo katika dakika ya 22 ya mchezo.
Kuingia kwa bao hilo kuliwamsha JKT Ruvu ambao nao walitulia na kuanza kucheza pasi fupi fupi, lakini uimara wa safu ya ulizi nya City iliyokuwa ikiongozwa na Deo Julius ulifanya kumalizika kwa kipindi cha kwanza City ikiwa Mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili vijana wa JKT Ruvu waliendelea kulishambulia lango la City wakitafuta bao la kusawazisha na jitihada zao zilizaa matunda kufuatia kupata bao katika dakika ya 60 , bao hilo halikudumu muda mrefu kwani Yohana Moriss alifanikiwa kuunganisha vizuri mpira wa kona uliopigwa na Hassan Mwasapili na kuipa City bao la pili ambalo lilihitimisha dakika 90 na kuifanya City kuibuka na ushindi wa 2-1.