Jumanne, 9 Februari 2016

Waziri Mwigulu Nchemba Amefika Eneo la Mapigano ya Wakulima na Wafugaji na Kuamuru Mambo Haya

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi takribani 200.
Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. 
 
Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima