Kambi ya upinzani Bungeni imeitaka serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu hatma ya mabehewa 274 ambayo yamenunuliwa na serikli kutoka nchini india yakiwa machakavu kwani yameligharimu taifa Bilioni 200 na iache kuyatumia ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kutokea.
Akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani katika wizara ya uchukuzi Mh.Moses Machali amesema mabehewa hayo yamelalamikiwa kwa kipindi kirefu lakini serikali imeendelea kuwa bubu.
Wakichangia Bajeti hiyo baadhi ya wabunge wamesema siyo sahihi kila Mwaka serikali inatenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali lakini haipeleki fedha hatua ambayo inarudisha nyuma maendeleo.
Kamati ya kutatua migogoro na kupambamana na ajali ambayo ipo Bungeni limesema kukabiliana na ajali kuna haja ya kuboreshwa zaidi kwa mipango iliyopo.
Awali akiwasilia Bajeti ya wizara yake Mh.Samweli Sitta amesema wizara yake inamikakati mbalimbali ya kuboresha sekta ya usafiri nchini ikiwemo kufufua sekta ya anga na reli ili kuhakisha maeneo yote yanafikika.