Jumanne, 26 Mei 2015
WASIMAMIZI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE KWA MAKUNDI MAALUM
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo –Chadema-dokta WILBROAD SLAA amewataka wasimamizi wa daftari la kudumu la wapiga kura kutoa kipaumbele kwa makundi maalum katika jamii ili waweze kujiandikisha bila kupata madhara.
Dokta SLAA ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Hamugembe wilayani Bukoba ambapo amesema kuwa kitendo cha kuwatengenezea mazingira bora wahusika wa makundi hayo kutarahisishia kutumia nafasi hiyo kutimiza malengo yao ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Mbali na hayo amemuagiza mwenyekiti wa Chadema Bukoba mjini VICTOR SHEREJEY kufuatilia katika vituo vyote na kuhakikisha kasoro zilizobainika zinafanyiwa kazi ikiwamo ya makundi hayo ya watu kuandikishwa bila kusumbuliwa.