Shirika la umeme Tanzania Tanesco katika kukabiliana na changamoto ya vitendea kazi limezindua magari ya kazi 132 yenye thamani ya shilingi bilioni nane pesa za kitanzania ambayo yamesambazwa katika wilaya zote nchini ikiwemo mikoa ya Mtwara na Lindi iliyokuwa na tatizo hilo.
Hafla fupi ya uzinduzi wa magari hayo kitaifa umefanyika mkoani
Mtwara huku mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Felchesmi Mramba alisema
magari hayo ni mapya yatasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta
ufanisi hasa wilayani, huku akisisitiza shirika hilo kuendelea
kujiboresha ili kuondoa malalamiko dhidi ya wananchi.
Akizungumzia uboreshaji wa kituo cha Mtwara na Lindi ambacho
kinazalisha mega wati 18 ambazo haziendani na uwekezaji uliyopo hivi
sasa anasema