Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC-pamoja na mjumbe wa SADC rais Jacob Zuma wamewasili nchni ili kutoa maamuzi ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchni Burundi.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere rais Uhuru Kenyata wa kenya ndiyo aliyekuwa wa kwanza kuwasili nchni ambapo alipokelewa na waziri wa Afrika Mashariki Dkt Harrison Mwakyembe na ungozi wa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, muda mfupi baada aliwasili mjumbe wa SADC ambaye pia rais wa Afrika Kusini Bwana Jocob Zuma naye amepata fursa ya kuangalia vikundi vya ngoma na brass band na kisha amewasili rais wa Uganda Bwana Yoweri Museveni ambaye kama ilivyo utaratibu kwa viongozi wakuu alipata fursa kuangalia ngoma na vikundi vingine vya burudani vilivyokuwa vikitumbwiza uwanjani hapo.
Akizungumza ,mwenyekiti wa mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe Dkt Harrison Mwakyembe amesema tayari mawaziri wa EAC na mawaziri wa mambo ya nje wameshakusanya taarifa mbalimbali zinazohusu mgogoro wa Burundi ambazo wametengeneza taarifa moja wanayoikabidhi kwa wakuu wa nchi ili kutoa uamuzi kuhsu mgogoro huo.
Aidha akizungumza kuhusu maamuzi ya rais Piere Nkurunziza ya kugombea kwa mara nyingine tena nafasi ya urais wa Burundi kwa madai ya uchaguzi wa kwanza haukuwa wa kuchaguliwa na wananchi mwenyekiti wa mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Harrison mwakyembe amesema.