Jumatatu, 1 Juni 2015

Chadema yasema itapinga vikali mswada wa sheria wa vyombo vya habari.


Chama cha Demokrasia na mandeleo Chadema kimesema kita hakikisha kina pinga vikali mswaada wa sheria wa vyombo vya habari unao tarajiwa kupitishwa bungeni usipitishwe, kwasababu una lenga kukandamiza vyombo vya habari vya watu binafsi.
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa Singida mashariki Mhesimiwa Tundu Lissu amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wilayani Ikungi, na kusema kuwa lengo la serekali ni kuwarudisha watanzania miaka ya nyuma, ili kuweza kuficha maovu yanayo tendeka ndani ya serekali kwa kutumia chombo kimoja cha taifa cha habari.
 
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Tundu Lissu amewataka wananchi wa jimbo la Singida mashariki kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa wingi, kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi mkuu kama jinsi walivyo fanikiwa kushinda katika uchaguzi wa serekali za mitaa kwa kupata ushindi wa zaidi viti arobaini huku CCM ikiambulia viti tatu.
 
Akiongea na maelfu ya wakazi wa jimbo la Singida mashariki waziri kivuli wa maliasili na utalii na mbunge wa Iringa mjini Mheshimiwa mchungaji Peter Simioni Msigwa, amesema baadhi ya viongozi wa CCM wame hujumu nchi kwa kutorosha maliasili nyingi hapa nchini, na kumekuwa na rushwa karibu katika sekta zote hata kusababisha huduma muhimu kama hospitali kukosa madawa, kutokana na hali hiyo Chadema imeamua kusimama imara na kutembea nchi nzima kuwaeleza wananchi na ili waweze kujua wachague chama gani katika uchagu mkuu unao kuja.
 
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na mamia ya wakazi wa jimbo la Singida mashariki wakiwemo wachungaji wa makanisa mbalimbali mashehe na wananchi wa jimbo hilo wameonyesha niayao ya kumrudisha mbunge wao kwasabau ya kuwatetea wananchi kuacha kuchangia michango maendeleo ambayo inatakiwa kutolewa na serikali.