Mamlaka
ya mawasiliano nchini TCRA kwa mara ya kwanza imeanza mpango wa ugawaji
wa masafa ya mawasiliano kwa njia ya mnada ili kuleta ushindani kwa
kampuni zinazotoa huduma ya mawasiliano kwa jamii ili yawe bora
kitechnologia na yenye wigo mpana kwa wananchi wote wa mijini na
vijijini.
Akizungumzia mpango huo jijini Dar es Salaam katika mkutano
uliowakutananisha wadau wa mawasiliano na mamlaka ya mawasialiano nchini
mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Profesa John Nkoma amesema kuwa TCRA
imeamua kufanya hivyo kutokana na ushindani mkubwa uliopo wa makampuni
ya mawasiliano nchini yanayopelekea masafa kuwa machache ukilinganisha
na makampuni yaliyopo jambo ambalo limelazimu uwepo wa uwazi katika
ugawaji wa masafa hayo ili kuwa chanzo cha kuliongezea taifa pato.
Kwa upande wake mhandisi wa masafa kutoka TCRA Bwana Victor Kweka
ameeleza kuwa licha ya kuwa mfumo huo wa ugawaji wa masafa kwa njia ya
mnada ni kwa mara ya kwanza nchini lakini utasaidia sana wananchi wa
vijijini kufikiwa na mawasiliano kutokana na masafa ya technologia mpya
kuhitaji minara michache kwa wigo mpana wa mawasiliano.
Mpango huo unatarajiwa kuanza kutumika October mwakani baada ya
wadau wote wa mawasiliano kushirikishwa ambapo kampuni ambazo zitashinda
kwa kufikia vigezo vitakavyowekwa katika mnada utakaotangazwa ndizo
zitakazo gawiwa masafa.