Jumanne, 26 Mei 2015

Baadhi ya wabunge wapinga serikali kuwa na sheria ambazo zinabinya uhuru wa habari.


Wakati wizara ya mawasiliano Sayansi na Teknoljia ikiwasilisha bajeti ya wizara yake baadhi ya wabunge wamepinga vikali sheria mbalimbali ambazo serikali imezipitisha ikiwemo ya miamala ya kieletoniki ya mwaka 2015 na sheria nya udhibiti wa uhalifu wa mtandao wa mwaka 2015 kuwa inafifisha uhuru wa watu kutoa taarifa mbalimbali ambazo zingeweza kusaidia kuharakisha maendeleo katika nchi.
Akiwasailisha bajeti ya wizara yake Mh Profesa Makame Mbarawa amesema wizara yake itahakikisha inaendelea kusimamia kwa kina sheria zilizopo ili kuona kuwa tekinolojia haitumiki vibaya.
Akizungumza kuhusu sheria hizo Mh Mchungaji Peter Msigwa amesema inashangaza kuona ni katika kipindi muhimu kama hiki ambacho watu wanahitaji kupata taarifa nyingi tena za uhakika alafu serikali inabinya uhuru wa wawatu kupata taarifa hizo.
Awali waziri wa viwanda na biashara Mh Abdallah Kigoda akiwasilisha bajeti ya wizaya yake amesema serikali inakusudia kutoa leseni kwa wamachinga wote ili waweze kufanya biashara katika mazingira tulivu. 
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge uchumi na biashara Mh Dunstan Kitandula amesema licha ya jitihada zinazofanywa na wizara lakini bado kuna tatizo kubwa katika uwepo wa viwanda nchini jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi.