Jumatano, 27 Mei 2015

Msichana alienyonga mtoto Morogoro amefikishwa mahakani.


Msichana Judith Chomile(15) amefikishwa katika hamakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro akikabiliwa na tuhuma za kumnyonga hadi kufa mtoto  mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi bernard benderi  ya mjini Morogoro
Akisoma shitaka mbele ya hakimu mkazi Ivan Msaki, mwendesha mashataka wa polisi Aminata Mazengo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo may 20 kinyume na kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu nahakutakiwa kujibu lolote  kutokana na kosa lenyewe na kuwa mtuhumiwa yuko  chini ya miaka 18 hivyo kuwakilishwa.
 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 10 mwaka huu itakapo tajwa tena mahakani hapo .
 
Katika hali isiyo ya kawaida ndugu wa marehemu Ediga Mafwere kwa hasira amempiga ngumi mtuhumiwa  muda mfupi baada ya kutoka mahakamani mbele ya maafisa wa jeshi la  polisi na ustawi wa jamii ambapo  naye alijikuta katika  mikono ya jeshi la polisi  na kufungwa pingu ambapo anashikiliwa kwa  mahojiano zaidi.
 
Akizungumza juu ya uhakika wa usalama wa msichana Judith Chomile afisa ustawi wa jamii manispaa ya Morogoro Jasmin Masenge amesema  msichana huyo atakuwa katika mikono salama chini ya uangalizi wa kitengo cha ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi kitengo cha dawati lajinsia na watoto hadi kesi inayomkabili itakapotolewa hukumu