Rais Dokta.Jakaya Kikwete amesema serikali yake ya awamu ya nne inaendelea kujitahidi kuhakikisha kuwa changamoto sugu zinazowakabili walimu zinapatiwa ufumbuzi na kuandaa mazingira bora ya kuiwezesha serikali ya awamu ya tano kukamilisha ufumbuzi wa changamoto zitakazobaki.
Dokta.Kikwete ametoa kauli hiyo ya matumaini kwa walimu wakati
akizungumza na walimu wawakilishi wa chama cha walimu nchini wanaokutana
jijini arusha.
Awali katika risala yake kwa rais,katibu mkuu wa CWT Alhaj Yahya
Msulwa aliziainisha changamoto wanazokabiliana nazo walimu kuwa ni
pamoja na maslahi duni,mazingira duni ya kazi na sua la upandishwaji wa
madaraja na marekebisho ya mishahara ambalo anasema kikwazo kubwa
kimekuwa ni watendaji hususani katika halmashauri za wilaya.
Mheshimiwa magreth sita ni mwenyekiti mstaafu wa CWT amesema ili
kuboresha elimu nchini ipo haja idara ya ukaguzi ikabadilishwa na kupewa
wakala ili kuongeza kasi ya utendaji huku waziri wa elimu dakta shukuru
kawambwa akitoa pongezi kwa CWT kwa kusaidia katika uboreshaji wa elimu
nchini.
Mkutano huo mkuu wa CWT unafanyika sambamba na uchaguzi mkuu wa
viongozi wa chama hicho katika ngazi ya kuanzia rais na makamu wake
,katibu mkuu na naibu wake pamoja na wajumbe.