Naodha wa timu ya chuma chakavu mbega daffa akipokea pesa taslimu kutoka kwa mgeni rasmi
Timu ya chuma chakavu leo hii imefanikiwa kushinda katika mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya timu ya ilemi fc timu ya taifa kipindi cha kwanza timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu zamu hadi mwamuzi anapiga kipenga cha kipindi cha kwanza kwenda mapumziko timu zote mbili zilikuwa azijafungana .kipindi cha pili timu zote mbili zilifanya mabadiliko huku timu ya chuma chakavu ikimtoa shabani mtupa nafasi yake ikichukuliwa na john matei na alen tingo alichukua nafasi ya dominick meshack na kwa upande timu ya ilemi fc ilimtoa paul henry akaingia hassan matitu na maganga ezekia alikwenda benchi nafasi yake ikichukuliwa na joseph mwangole na kufanya mchezo kipindi cha pili kuwa mzuri na timu ya ilemi fc kufanya mashambuli ya mara kwa mara dak 58 ya kipindi cha pili alen tingo akapachika goli la ushindi kwa timu ya chuma chakavu.kesho ligi inaanza kwa kuzikutanisha timu ya felali fc na mafiati fc usikose kufuatilia mitanange hii ya dasani mastala cup yaliyodhaminiwa na cocacola kwanza kupitia maji ya dasani.