Jumapili, 26 Aprili 2015

TANZANIA PRISONS YAWAFUTA MACHOZI KIDOGO MASHABIKI WAKE



Ligi kuu ya vodacom imeendelea leo kwa michezo miwili katika mikoa ya Morogoro na Mbeya, ambapo mkoani Mbeya kushuhudia Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa Mgambo shooting na Morogoro Mtibwa sugar wakiwa Wenyeji wa JKT Ruvu.

Katika uwanja wa Manungu uliopo Turiani Morogoro, Mtibwa Sugar wamekubali kichapo cha goli 1-0 toka kwaJKT Ruvu.

Goli la JKT Ruvu lilipatikana katika kipindi cha pili baada ya Mtibwa sugar kujifunga na kuizawadia point tatu JKT Ruvu, ambao wamefikisha pointi 28.

Katika uwanja wa Sokoini mkoani Mbeya, Tanzania Prisons wamefanikiwa kujikusanyia pointi tatu baada ya kuwachapa Mgambo shooting goi 2-0.

Goli zote za Tanzania Prisons zilipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo, na hivyo matokeo hayo yanaifanya ifikishe pointi 25 n kusogea kwa nafasi mbili toka katika nafasi ya 14 maka nafasi ya 12 katika msimanmo wa ligi kuu ya vodacom.