Jumapili, 19 Aprili 2015

TZ PRISON WALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR

Image result for TZ PRISONSTanzania Prisons na Mtibwa sugar hii leo wamegawana pointi baada ya kwenda sare ya goli 1-1 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.
Katika kipindi cha kwanza timu zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu huku wachezaji wakipoteza umakini katika kupiga pasi, ambapo wachezaji wakati watimu zote mbili walikuwa wakipoteza mipira kirahisi.

Katika dakika ya 40 kona ya Said Mkopi ilituwa katika kichwa cha Mussa Mgosi, ambacho kiligonga mwamba na kumkuta tena Mgosi na kuipatia Mtibwa Sugar goli la kuongoza, na kuipeleka Mtibwa sugar mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilikuwa tofauti kidogo na kipindi cha kwanza ambapo wachezaji wa eneo la kiungo waliongeza umakini na kupelekea upande zote mbili kutengeneza nafasi kadhaa za kujipatia magoli.

Katika dakika ya 77 Amiri Omary alifanyajaribio na kumtoka Andrew Vicent, Vicent alimchezea madhambi na kuzaa penati ambayo ilipigwa kifasaha na Lugano Mwangama na kuipatia Tanzania Prisons goli la kusawazisha na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.