Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo imeanza mazoezi katika uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamka kama (Haille Sellsie) uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.
Stars ambayo iliwasili jana jioni jijini Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo iliyopo eneo na 22 Mazoiria ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapharao.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema anashukuru vijana wake wamefika salama, na wapo katika hali nzuri, anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia itasaidia kikosi chake kuwa fiti ajili ya mchezo.
Kuhusu hali ya hewa ni nzuri kwani baridi iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo haitaweza kuwasumbua wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.