Jumatatu, 11 Mei 2015

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA NAFASI KATIKA USHINDANI WA BIASHARA KATIKA SOKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


WAZIRI wa Afrika Mashariki Dokta HARRISON MWAKYEMBE, amesema endapo Watanzania hawatachangamkia fursa katika Ushindani wa biashara kwenye Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, watakuwa Bingwa wa kuchukua Kombe la usindikizaji kwa nchi jirani.
Amesema Tanzania ina fursa kubwa za kufanyabiashara nje ya nchi, lakini bado iko nyuma na imeshuka katika kupeleka bidhaa nje ya nchi kutoka Asilimia 18.8 mwaka 2000 hadi Asilimia 4 mwaka 2014.
Waziri MWAKYEMBE amesema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Mara katika Mji mdogo wa Sirari ambapo amezungumza na wafanyabiashara na Wakulima katika mji huo.