Jumamosi, 1 Agosti 2015

RAFU ZATAWALA KWENYE KURA ZA MAONI MOJA YA WAGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM AMEANDAA VIJANA KWA AJIRI KUWAFOSI WATU WAMPIGIE KURA MKOANI MBEYA WENZAKE WASEMA HAWAKO TAYARI NA MATOKEO YAKE KIKAO KIZITO CHAITISHWA HIVI SASA OFISI ZA CCM MKOA..



Wakati zoezi la uchaguzi wa kura  za maoni kuchagua.mbunge na madiwani jimbo la mbeya mjini likiendelea, rafu zimeendelea mapema leo katika vituo vya kupigia kura.

Mmoja wa wagombea adaiwa kuandaa kundi la vijana ndani ya ccm kuwalazimisha kumpigia kura.

Blogu hii imeshuhudia malalamiko hayo katika kata za Iyela katika kituo cha muungano, Iyunga na manga anbapo vijana hao walikuwa wakiwatisha makada wenzao kupiga kura kwa namba ya mgombea huyo.

Wagombea wenzake wajipanga kususia kumuunga.mkono kwenye kampeni kama jina lake litarudi kutokana na viongozi kuonekana kutaka.kumbeba.

Mmoja wa viongozi waandamizi wa jumuia ya vijana UVCCM adaiwa kuhojiwa na Takukuru baada ya kukutwa akigawa fedha za mgombea huyo jana usiku.