Jumatano, 1 Julai 2015

DI MARIA SHUJAA AFANYA YAKE DHIDI YA PARAGUAY


TIMU ya taifa ya Argentina imetinga fainali ya Copa America 2105 baada ya kuifunga Paraguay mabao 6-1 usiku wa kuamkia leo mjini Concepcion, Chile.
Kwa ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya winga wa Manchester United, Angel di Maria na mengine ya Marcos Rojo, Sergio Aguero, Javier Pastore na Gonzalo Higuain, Argentina itakutana na wenyeji Chile katika fainali.