Ajali hiyo imetokea baada ya basi la kampuni ya Super Feo likiwa
kwenye mwendo mkali kujaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake, lakini
kabla halijafanikiwa kulipita kwa mbele likatokea lori la mafuta, hali
ambayo ikasababisha dereva wa basi kulikwepa kwa upande wa kulia, lakini
akashindwa kulimudu na ndipo lilipopoteza mwelekeo na kutumbukia mtoni.
Daktari wa zamu katika hospitali ya rufaa Mbeya, Dk Lathan Mwakyusa
amethibitisha kupokea miili ya watu watatu pamoja na majeruhi 28
wanaotokana na ajali hiyo.
Kwa upande wake afisa mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Mbeya, Denis
Daudi amesikitishwa na ajali hiyo na kuwataka madereva kuongeza umakini
wawapo barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.