Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imekamata vipodozi katoni 45 pamoja na maziwa yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu Box20 vililvyokuwa vikisafirishwa kinyume na sheria katika basi la Taqwa kutoka kampala nchini uganda kwenda jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kukagua basi hilo mkaguzi wa TFDA kanda ya
mashariki Dokta. Ediga Mahundi amesema walipata tarifa za siri kutoka
kwa wasamaria wema ambapo waliweka mtego katika mzani wa Kihonda mjini
morogoro na kufanikiwa kukamata vipodozi hivyo huku ameeleza vipodozi
hivyo havifai kwa matumizi ya binadamu na vimekuwa vikisababisha tatizo
la watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa na.
Katika hali isiyo ya kawaida abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi
hilo wameonekana kunywa maziwa yaliyokamatwa na mamlaka ya chakula na
Dawa wakidai maziwa hayo ni salama kwa matumizi ya binadamu na wame
zitaka mamlaka husika kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri kabla ya
kuigia nchini.