Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk Wilibroad Slaa amewataka watanzania kupiga na kutokubali mswaada wa sheria unaotaka kupitishwa na serikali wa kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na kuwanyima watanzania haki na uhuru wa kupata habari.
Akiongea na wananchi mjini Bukoba katibu mkuu wa chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema Dk Wilibroad Slaa amewataka watanzania
kutokukubali sheria hiyo ambayo inalengo la kuwanyima watanzania haki na
uhuru wa kupata habari na kwamba sheria hiyo ikipitishwa watanzania
wataendela kubaki gizani na kuishi kama waposhimoni bila kuelewa maovu
yanayofanywa na viongozi wasio waadilifu wanaotumia madaraka vibaya kwa
masalahiyao binafsi.
Hata hivyo katibu mkuu wa chama demokrasia na maendelio Chadema Dk
Wilibroad Slaa amesema nia ya serikali kutaka kuzuia uhuru wa vyombo vya
habari ni kuwarudisha nyuma watanzania ili waweze kuishi bila kupata
habari kama ilivyokuwa enzi za ukoloni nakwamba haliyo haiwezi
kuvumiliwa kwani serikali inataka kuficha maovu ambayo
yanawekuliangamiza taifa hapo baadae.