Jumanne, 2 Februari 2016

Mzozo Mkubwa Waingia Kati ya Jiji na Madereva Daladala


Jiji la Mbeya na Madereva Daladala wamejikuta wakiingia katika Mgogoro Ambao Umefika mpaka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya .Mh Abass Kandoro na Kuitisha kikao cha Dhalula Ambacho kilimalizika kwa Maadhimio kuwa daladala zote zinazotoka Stendi kuu kwenda Uyole njia itakayokuwa inatumika kwa Daladala ni njia ya Rift Valley Hotel na kukatishia  njia ya Nmb Bank.Baaada ya kuulizwa Maswali na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa akuelezea sababu za Msingi za Kukataza Barabara ya Karume Road Hata hivyo Mtandao huu Umebaini  barabara ya Rift valley ni Barabara ambayo sio nzuri kama unavyojionea hapo juu kwenye picha.Akiongea na Vyombo vya habari Kandoro Alisema Serikali itajenga barabara ya kutokea Iganzo kwenda Kabwe kwa njia ya Lami hivi karibuni.Hata hivyo kauli hiyo imeonekana kugomewa na madereva hiace hao kuwa barabara wanayopelekwa kwa sasa bado ni mbovu hadi mtandao huu unaondoka ulikuwa umewaacha madereva hao katika ofisi za mkuu wa mkoa.