Vurugu kubwa zimetokea katika mji wa
Njombe mkoani Njombe baada ya Basili Mwalongo mkazi wa mkoani humo
kuuawa kwa kupigwa na polisi jana usiku ambapo wananchi wameandamana
katika hospitali ya mkoa wa Njombe ambapo polisi wamelazimika
kuwatawanya kwa risasi na kujeruhi wananchi kadhaa huku baadhi ya maduka
yakifungwa na shughuli kusimama.
Mwandishi wetu ameshudia wananchi wakiwa wameandamana na kufunga barabara huku
wakiwasha matari barabarani wakiwa wameshika chupa za maji kukabiliana
na mabomu ya machozi ambapo Mwandishi wetu amezungumza na majeruhi wa kadhia hiyo Fredy
Sanga akiwa amejeruhiwa kwa kupigwa risasi sehemu za siri na Lupiana
Mandela aliyejeruhiwa kichwani.
Diwani wa kata ya Njombe mjini Bw. Agrey Mtambo aliyejaribu kuwatawanya wananchi hao bila mafanikio amekuwa na haya ya kusema.
Kufuatia vurugu hizo polisi mkoani Njombe wamelazimika kupiga
mabomu ovyo kutwanya mikusanyiko ya watu huku kamanda wa polisi wa mkoa
wa Ruvuma Bw.Franco Kibona akigoma kuzungumza na waandishi wa habari kwa
madai kuwa hawezi kuzungumza wakati vurugu zikiendelea halikadharika
madaktari katika hospitali ya mkoa wa Njombe wakigoma kuzungumza.