Jumanne, 19 Mei 2015

SERIKALI YAWAASA VIJANA KUJIEPUSHA NA NGONO ZEMBE PAMOJA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA


SERIKALI imewaasa vijana kujiepusha na ngono zembe ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya  dawa zakulevya ili waweze kujiletea maendeleo yao na kujiinua kiuchumi.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa mafunzo elekezi ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana  wa halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Amesema vijana kujihusisha na ngono Zembe na Matumizi ya Dawa za kulevya kutawafanya kuwa dhaifu na kushindwa kuchangia katika Ujenzi wa taifa na kujiinua kiuchumi