Siku ya jumapili haikua nzuri kwa familia ya Hip hop Marekani, baada
ya rapper anaetokea katika familia ya French Montana ya Coke Boys kuuawa
kwa kupigwa risasi mfululizo.
Anajulikana kama Chinx Drugs(31), akiwa ndani ya gari mitaa ya Qeens
Boulevard ilitokea gari jirani yake na kushambuliwa kwa risasi mfululizo
iliyopelekea mauaji hayo.
Chinx Drugs ameshafanya kazi na stars wa hip hop wakubwa duniani,
kama French Montana aliyekuwa nae kundi moja na billionare Pdidy.