Serikali imepanga kujenga nyumba 4,036 ili kukabiliana na uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi wa nyumba za wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani
Hayo
yamesemwa leo na Naibu waziri wa mambo ya ndani Hamadi Masauni
alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Momba Mkoani Mbeya David
Silinde (CHADEMA) aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutatua
kero kuu ya askari polisi kukosa nyumba za kuishi pamoja na ofisi za
kufanyia kazi.
''Mheshimiwa
Spika Serikali inatambua uhaba mkubwa wa nyumba za watumishi wa nyumba
za wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani hasa askari polisi.
"Ili
kutatua tatizo hilo tumejipanga kupata mkopo kutoka benki ya Exim China
ili kujenga nyumba 4,036 za polisi katika maeneo ambayo yana uhaba
mkubwa zaidi nchini''. Amesisitiza Masauni.
Aidha Serikali imesema nyumba hizo zitahusisha pia upande wa Unguja na Pemba katika mgawanyo utakao kwenda kwa awamu mbalimbali.