Pichani ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye leo ameapishwa rasmi kuanza kupambana na majangili ambao wamekuwa kero kwa nchi hii.
Ikumbukwe kuwa kuna wakati Tanzania ilifikia kuwa kinara cha matukio ya ujangili kiasi cha Serikali ya Awamu ya Nne kuanzisha Operesheni Tokomeza ambayo nayo haikuisha vizuri.
Maliasili ya Tanzania ikitunzwa vizuri inaweza kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa nchi ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi kupitia utalii.
Tunakutakia kila la heri katika majukumu yako mapya Meja Jenerali Gaudence Milanzi.