Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), leo Juni 7, 2016 limefanya
kikao cha pamoja na uongozi wa Klabu ya Young Africans.
Kikao hicho kilifanyika ofisi ya TFF iliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Ilala jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi
kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine; Kaimu Mkurugenzi wa
Sheria na Uanachama, Elliud Mvella; Makamu Mwenyekiti wa Young Africans,
Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Young Africans, Baraka Deusdedit.
Baada ya mazungumzo, Rais wa TFF, Malinzi ametoa maelekezo yafuatayo:-
1.
Mchakato
wa Uchaguzi wa Young Africans uendelee.
2.
Mchakato
huo usimamiwe na Kamati ya Uchaguzi ya Young Africans chini ya uangalizi wa
Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
3.
Wale wote waliochukuliwa fomu za uchaguzi wa
Young Africans katika ofisi za TFF washirikishwe kwenye mchakato huo.
Mwisho, Rais wa TFF Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wanachama na wapenzi wa Young Africans na kuwa na umoja na
mshikamano kuelekea uchaguzi huo muhimu wa kwa mustakabali wa klabu.