Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Afisa wa idara ya usafirishaji na mazingira jiji, Samuel Bubegwa akielezea jinsi kuwa taasisi zitakazoshiriki kwenye zoezi la usafi(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Waandishi wa Habari wakimskiliza Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
NA SAMWEL NDONI MBEYA,
WATUMISHI wa serikali,sekta binafsi na makampuni mbalimbali jijini hapa wanatarajia kuadhimisha siku ya uhuru kwa kufanya usafi kwenye maeneo waliyoelekezwa na halmashauri ya jiji ikiwa ni utekelezaji wa wa agizo la raisi Dr. John Magufuli.
Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr. Samwel Lazaro amesema kuwa kwa sasa jiji la Mbeya linachangamoto ya kuwa na uchafu mwingi kutokana na mfumo wa ukusanyaji taka unaotumika sasa
Amesema halmashauri iliondoa maghuba na kuanzisha mfumo wa wananchi kukusanya taka wanazozalisha kwenye maeneo yao na kutoa utaratibu kwa magari ya kuzoa taka kupita kwenye maeneo hayo na kuziondoa taka hizo.
‘Changamoto tunayoipata kwenye mfumo huu ni baadhi ya watu wanakusanya takataka kwenye maeneo ya wazi kama vile barabarani hali iliyopelekea maeneo mengi ya wazi kuwa machafu na hasa wakati huu wa mvua’’ amesema
Amesema halmashauri ya jiji kwa sasa imeelezeza nguvu kwenye suala la usafi ambapo tayari wamefanya usafi mkubwa kwenye soko la Soweto na kwamba utaratibu wa kufanya usafi utakuwa mara moja kwa wiki.
Dr. Lazaro amesema siku ya disemba 9, watumishi wa halmashauri wataadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi kuanzia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya mpaka kwenye kituo kikubwa cha mabasi na kuwataka madereva wote kuwa na vyombo maalum vya kuhifadhia taka.
Afisa wa idara ya usafirishaji na mazingira jiji, Samuel Bubegwa amesema kuwa taasisi zitakazoshiriki kwenye zoezi la usafi kwenye maeneo yao na maeneo mengine ni benki ya NBC, TTCL, kampuni ya simu ya Airtel na vyuo vya Saut na TEKU pamoja na walimu wa shule ya sokondari Sangu.
Wengine ni wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga, askari Magereza, polisi wafanyakazi wa benki kuu, viongozi wa wilaya, wafanyabiashara wa masoko ya Sido na Soweto pamoja na chama cha Mapinduzi CCM.
Aliongeza kuwa wafanyakazi wa Hospitali ya rufaa Mbeya na hospitali ya wazazi meta wameelekezwa kufanya usafi ndani ya Hospitali na maeneo yanayozunguka.
mwisho