Rais
Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa mjumbe maalum mpya wa Umoja
wa Afrika (AU) kwenda nchini Libya akichukua nafasi ya Dileita Mohamed
Dileita wa Djibouti aliyeishika nafasi hiyo tangu mwaka 2014.
Uteuzi
huo uliofanywa na Umoja wa Afrika katika kikao chake kilichofanyika
jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kimeuelezea kuwa sehemu ya juhudi za
Umoja huo katika kuhakikisha inarudisha hali ya usalama na amani nchini
Libya.
Kamishna
wa Amani na Usalama wa AU, Smail Chergui jana alitangaza uteuzi huo
alipokuwa anatoa muhtasari wa majadiliano na makubaliano ya kikao hicho
killichowakutanisha viongozi wa ngazi za juu wa nchi wanachama.
Libya imekuwa katika machafuko tangu kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.