Kada wa CCM na mjumbe wa NEC, Charles Mwakipesile leo ameongea na waandishi wa habari katika hotel ya hill view na kuweka bayana kuwa pamoja katika kampeni na Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Sambwee Shitambala.
Akiongelea kuhusu kukosa nafasi ya kuwakilisha jimbo la mbeya mjini amewashukuru Wananchi wa jimbo la mbeya mjini kwa kuonesha upendo kwake . na kuishukuru kamati kuu ya CCM kwa uteuzi wa shitambala.
Mwakipesile alisema makundi yote yaliyokuwa katika kipindi cha kutafuta mgombea mmoja ndani ya chama walikaa pamoja na kukubali kwa pamoja na kufuta makundi yaliyokuwepo ndani yao.
Akiulizwa swali na mtandao huu kuhusu kukubali kwa moyo wa dhati kwa wagombea wengine kati ya kumi waliosaini kuvunja makundi alisema kama kuna mtu ana chuki kwa sababu ya kutochaguliwa na chama atabaki na chuki yake mwenyewe.