Jumatatu, 24 Agosti 2015

MGOMBEA URAIS KUPITIA UKAWA EDWARD LOWASSA LEO AFANYA ZIARA KWENYE DALADALA NA MAMA LISHE JIJI DAR

Mgombe Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) ambae pia anaungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA Mh. Edward Lowassa akimsikiliza mmoja wa mama ntilie anayeuza mihogo katika eneo la kituo cha Daladala Gongo la mboto mwisho, alipokuwa kwenye ziara ya kujionea shida ya usafiri wa umma na kusiiliza kero mbalimbali za wakazi jiji la Dar es Salaam leo asubuhi
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Edward Lowassa akilipa nauli yake ndani ya daladala iliyotoka Gongo la mboto mwisho hadi Chanika lenye namba T 917 CWS wakati alipofanya ziara ya kujionea hali ya matatizo ya usafiri wa Umma katika jiji la dar es Salaam
Mgombe Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia anaungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA Mh. Edward Lowassa akiongea na wanafunzi aliowakuta Kituo cha basi Gongo lamboto mwisho wakisubiria usafiri kuelekea shuleni katika, Huku mmoja wa wanafunzi hao akimwonyesha kadi ya kupigia kura.