Watu wawili wamejeruhiwa na zaidi ya kaya 78 zimeezuliwa na mvua kubwa yenye upepo mkali iliyonyesha katika kijiji cha Kasoto wilayani Geita.
Mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa nane mchana kukatika baada ya masaa matatu imeezua paa na nyumba 17 kubomoa kabisa hivyo kukosa kabisa mahali pa kuishi.
Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Omary Mangochie ametembelea kijijini hapo na kujione uharibifu wa majengo na kumtaka mhandisi wa wilaya ya Geita kufanya tahimini ya uharibifu uliuojitokeza, aidha amewataka baadhi ya wananchi kuwasaidia wale waliopatwa na maafa.