Jumatano, 3 Juni 2015

WEMA SEPETU AWASHUKIA WAANDAJI WA INSTAGRAM PARTY ,KISA MALIPO YA MZEE MAJUTO

Staa wa Bongo Movies Wema Sepetu ameamaua kuwachana wazi wazi waandaaji wa Instagram Party kwa kitendo chao cha kutomlipa pesa hadi sasa hivi staa mwenzake Mzee Majuto.
Waandaaji wa Instagram party sijawapenda kiukweli. Mpaka nimefkia hatua ya kuandika basi mjue kuwa mmenikwaza. Mlikuja kwangu na mkaniomba
niwatafutie Huyu Mzee wa watu... Kwa moyo mmoja nilifanya hivyo, Iweje leo hii kashamaliza kazi msitake kumlipa hela yake... Baba wa watu katoka Tanga na nauli yake, mpaka hotel kajilipia mwenyewe.... Mimi sipendi lawama jamani... Sana sana ikiwa ni kwa wasanii wenzangu.