Jumatano, 3 Juni 2015

Mh.Mwakyembe asikitishwa na watu wanaotumia jina lake kuchafua watu kupitia mitandao ya kijamii.

Waziri wa ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mh Harrison Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na kufedheheshwa na kile alichokiita kuwa ni tabia ya baadhi ya watanzania kutokuwa majasiri na kutumia majina ya watu wengine kutoa maoni ama misimamo yao kufuatia taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii inayodaiwa kutolewa na waziri huyu kuhusiana na sakata la Richmond lililomlazimu waziri mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa kutoka madarakani.
HARUBUTZ imefika katika ofisi za waziri huyo kutaka kufahamu ukweli wa taarifa hizo ambapo Mh Mwakyembe amekanusha kuhusika na kuongeza kuwa suala hilo si lake bali ni maamuzi ya bunge na kwamba suala la Richmond lilifungwa miaka saba iliyopita.
 
Pia waziri huyo pia amezungumzia hatua alizozichukua na kubaini kuwa waliohusika baadhi yao ni viongozi wa dini na wafanyakazi wanaoheshimika katika baadhi ya wizara na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika watawekwa hadharani ili liwe fundisho kwa wengine.