Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, Ernest Mangu akizungumza
na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar
es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi na raia wa eneo hilo
kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia
leo.
Viongozi wa Jeshi la Polisi
nchini wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, Ernest Mangu, wakitembelea maeneo mbalimbali ambayo majambazi walidhuru, katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
ASKARI wa nne wa Jeshi la Polisi na raia watatu wamefariki dunia
katika tukio la ujambazi lililotokea katika kituo cha Polisi cha
Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam
Katika tukio hilo watu wapatao nane wamesadikika kuingia
katika kituo hicho cha Polisi eneo la Stakishari majira ya saa 4 usiku wa
kuamkia leo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, Ernest Mangu amesema lengo la la watu hao ni kutaka kuiba silaha
zilizokuwa katika kituo hicho cha Stakishari.
Aidha, amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa
taarifa zinazohusu uharifu kwa Jeshi la Polisi.
Pia, kuhusu uvamizi wa Majambazi, Mangu amesema watajitahidi
kuanza kuimarisha ulinzi kwa upande wao hususani katika vituo vya Polisi ndiyo
baadae kwenda kuimarisha usalama wa wananchi.