Jumapili, 7 Juni 2015

BARCELONA MABINGWA UEFA 2015

Klabu ya FC Barcelona imefanikiwa kutwaa kombe la tano la Uefa Champions League baada ya kuishushia kipigo cha mabao 3-1 Juventus katika mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa iliyopigwa usiku wa jana kwenye uwanja wa Olympic jijini Berlin, Ujerumani.
Barcelona walianza mchezo huo kwa kasi ambapo katika dakika ya tatu, Ivan Rakitic aliandika bao la kwanza akimalizia pasi safi ya Andres Iniesta hivyo Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Katika Kipindi cha pili Juventus walisawazisha bao hilo kupitia kwa Alvaro Morata aliyemalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Barcelona.
Hata hivyo katika Dakika ya 68 Lionel Messi alipiga shuti kali lililotemwa na mlinda mlango wa Juventus na mpira kumkuta Luis Suarez aliyefunga goli pili na katika Dakika za nyongeza Neymar aliifungia Barcelona goli la tatu la ushindi.
Vikosi vilikuwa:
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Barzagli, Evra, Marchisio, Pirlo, Pogba, Vidal, Tevez, Morata.
Benchi: Storari, Ogbonna, Coman, Llorente, Padoin, Sturaro, Pereyra.
Barcelona: ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Messi, Neymar, Suarez.
Benchi: Bravo, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Adriano, Mathieu.
Mwamuzi wa kati: Cuneyt Cakir