Alhamisi, 21 Mei 2015
SERIKALI NA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZATAKIWA KUWA WAZI.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Serikali na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali Barani Afrika zimetakiwa kubadili maudhui yake kwa kuweka mipango ya uendeshaji wa mambo yake kwa uwazi hasa kwenye sekta za uchumi. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),George Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali Barani Afrika kutoka serikalini na Taasisi zisizo za kiserikali,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijijini Dar es Salaam leo.
Mkuchika amesema kuwa,mkutano huo utasaidia sana endapo yaliyozungumzwa kwa siku mbili katika mkutano huo yatafuatwa na wananchi wataweza kujua mambo mbalimbali katika nchi zao, pia kila mwananchi ashiriki vyema kufanikisha malengo ya nchi.
Pia kwa upande wa serikali amesema kuwa serikali ikiweka mambo yake kwa uwazi pia inaweza kukosolewa, sio kila jambo inalofanya ni sahihi inahitaji kukosolewa ili kuleta maendeleo, pia wananchi waweze kufahamu nini kinaendelea katika nchi husika.