Walioapishwa ni:
Balozi Mahadhi Juma Maalim, ambaye anakuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kuwait.
Luteni
Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, ambaye anakuwa Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akijaza nafasi iliyoachwa wazi na
Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba, ambaye amestaafu. Kabla ya Uteuzi
huu Luteni Jenerali Mabeyo alikuwa Mkuu wa Usalama na Utambuzi wa Jeshi
la wananchi Tanzania.
Kamishna
Paul Moses Chagonja, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,
akijaza nafasi iliyoachwa wazi Madeni Kipande ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Kamishna
Clodwig Mathew Mtweve, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,
akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Akizungumza
baada ya kuapishwa, Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kuwait Mheshimiwa
Mahadhi Juma Maalim, ameahidi kuiwakilisha vyema Tanzania nchini Kuwait
hususani katika uchumi ili Tanzania iweze kunufaika na ushirikiano
uliopo baina ya mataifa haya mawili.
Nae
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa wananchi Tanzania Luteni Jenerali Venance
Salvatory Mabeyo, ameahidi kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na
Mtangulizi wake Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Albert Ndomba ya
kuhakikisha anamshauri vizuri Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na hivyo
kuliwezesha Jeshi hilo kutekeleza wajibu wake ipasavyo.
Kwa
upande wao, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna Clodwig Mathew
Mtweve na Katibu wa Mkoa wa Katavi Kamishna Paul Moses Chagonja,
wameahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kusukuma gurudumu la
maendeleo kwenye mikoa waliyopangiwa, ikiwemo kusimamia nidhamu kwa
watumishi wa umma.
Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
30 Januari, 2016