Ijumaa, 8 Januari 2016

Serikali Yatoa Picha Rasmi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufuli

Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.
Kila nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu.  Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano tu.  Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
 

Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi.  Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.
Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza  picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.

Hatua za kisheria  zitachukuliwa dhidi yao.  Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.