Ijumaa, 29 Januari 2016

Serikali yasema Aitamuonea Huruma Mkwepa Kodi

Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa  mapato ya ndani ya kodi na ambayo siyo kodi ni lazima yakusanywe kikamilifu kwa mujibu wa sheria bila upendeleo na kuwaonea huruma wakwepa kodi nchini.

Mhe. Mpango ameyasema hayo kwenye mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni Mjini Dodoma alipokua akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizochangia na kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja tarehe 20 Novemba 2015 .

Dkt. amesema ni lazima watumishi na walipa kodi kufanya majukumu yao kikamilifu ili kupata fedha ambazo zitawasaidia wananchi wa vijijini kupata maendeleo kwa kupata huduma muhimu.