Alhamisi, 28 Januari 2016

MH.MARY MWANJELWA MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA MBEYA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII

Wabunge wa Bunge la Kumi na Moja wamewachagua Wenyeviti wa tatu wa Bunge ambao watasaidiana na Spika wa Bunge na Naibu Spika katika kuliongoza Bunge la Kumi na Moja katika kipindi cha Nusu ya Uhai wake.

Waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo Mhe. Andrew Chenge (MB), Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Dr Mary Mwanjelwa (MB) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba Mhe.Najma Giga (MB).


Akizungumza kabla ya uchaguzi wa Wenyeviti hao Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah alisema Kamati ya Uongozi iliwapitisha Wabunge watatu kugombea nafasi hizo tatu za Uenyekiti wa Bunge.
Dkt Kashililah alisema kwa kuwa Wagombea waliopitishwa ni watatu na kwa kuwa nafasi zilikuwa tatu hivo Bunge lilikuwa na kazi ya kuwadhibitisha.

Hivyo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai aliwaita Wagombea wote watatu kujinadi mbele ya Bunge kabla ya kupigiwa kura ya pamoja ya Ndio au Hapana.

Ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo Mhe. Andrew Chenge (MB), Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Dr Mary Mwanjelwa (MB) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba Mhe.Najma Giga (MB) walichaguliwa kwa kura nyingi za Ndio kuwa Wenyeviti wa Bunge.