Jumanne, 17 Novemba 2015

JOB NDUGAI NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma wamemchagua  mheshimiwa  Job Yustino Ndugai kuwa spika wa bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Katibu wa Bunge Mh Dkt Thomasi Kashilila Amemtangaza Mh Job ndugai  kuwa Spika wa Bunge la 11 baada ya Kujinyakulia Kura 254 sawa na 70% ya Kura zote zilizopigwa.