Jumatatu, 16 Novemba 2015

Watu 5 waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu Nyangarata waokolewa wakiwa hai.

KWA HISANI YA ITV HABARI

Hatimaye wachimbaji wadogo watano waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu ya Nyangalata tarehe tano ya mwezi wa kumi wameokolewa wakiwa hai baada ya kukaa chini ya ardhi kwa takribani siku arobaini na moja huku mwingine wa sita akiwa 
tayari kashapoteza maisha.

Ni jambo ambalo sio rahisi kuingia akilini na kueleweka binadamu kukaa chini ya ardhi kwa zaidi ya siku arobaini lakini watu hawa watano walijikuta wakiishi kwa kudura za mwenyezi mungu .

Aidha mganga mfawidhi wa hospitali ya Kahama Dr.Joseph Ngowi amethibitisha kupokea wahanga hao wakiwa hai huku mmoja wa mashuhuda aliyefanikisha watu hao kuokolewa akisimulia jinsi alivyogundua uwepo wa watu chini ya ardhi.

Kwa upande wake katibu mkuu wa wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Bw. George Kibusy ametoa rai kwa yeyote atakayeguswa kutoa masaada wa hali na mali kwakuwa wahanga hao wana mahitaji makubwa ikiwemo nguo na chakula.