Ijumaa, 8 Mei 2015
MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR HUENDA ZIKALETA MADHARA MBALIMBALI
MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam, zimeelezwa kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo baadhi ya madaraja kukumbwa na maji, barabara kutopitika na hata baadhi ya magari kuchukuliwa na maji.
Mwandishi wa harubutz amezunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo ameshuhudia baadhi ya karavati zimesombwa na maji huku msongamano wa magari ukiwa ni mkubwa katika barabara zote za jiji.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliozungumza na harubutz, wamelalamikia tatizo la miundombinu mibovu lililopo katika jiji hilo.